4 Nawe utajifurahisha kwa BWANA,Naye atakupa haja za moyo wako.
5 Umkabidhi BWANA njia yako,Pia umtumaini, naye atafanya.
6 Ataitokeza haki yako kama nuru,Na hukumu yako kama adhuhuri.
7 Ukae kimya mbele za BWANA,Nawe umngojee kwa saburi;Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake,Wala mtu afanyaye hila.
8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu,Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
9 Maana watenda mabaya wataharibiwa,Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.
10 Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo,Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.