1 Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako,Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako.
2 Kwa maana mishale yako imenichoma,Na mkono wako umenipata.
3 Hamna uzima katika mwili wanguKwa sababu ya ghadhabu yako.Wala hamna amani mifupani mwanguKwa sababu ya hatia zangu.
4 Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa,Kama mzigo mzito zimenilemea mno.
5 Jeraha zangu zinanuka, zimeoza,Kwa sababu ya upumbavu wangu.