18 Kwa maana nitaungama uovu wangu,Na kusikitika kwa dhambi zangu.
19 Lakini adui zangu ni wazima wenye nguvu,Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi.
20 Naam, wakilipa mabaya kwa mema,Huwa adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema.
21 Wewe, BWANA, usiniache,Mungu wangu, usijitenge nami.