5 Jeraha zangu zinanuka, zimeoza,Kwa sababu ya upumbavu wangu.
6 Nimepindika na kuinama sana,Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika.
7 Maana viuno vyangu vimejaa homa,Wala hamna uzima katika mwili wangu.
8 Nimedhoofika na kuchubuka sana,Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu.
9 Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako,Kuugua kwangu hakukusitirika kwako.
10 Moyo wangu unapwita-pwita,Nguvu zangu zimeniacha;Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.
11 Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu;Naam, karibu zangu wamesimama mbali.