4 BWANA, unijulishe mwisho wangu,Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani;Nijue jinsi nilivyo dhaifu.
5 Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri;Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako.Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
6 Binadamu huenda tu huko na huko kama kivuli;Hufanya ghasia tu kwa ajili ya ubatili;Huweka akiba wala hajui ni nani atakayeichukua.
7 Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana?Matumaini yangu ni kwako.
8 Uniokoe na maasi yangu yote,Usinifanye laumu ya mpumbavu.
9 Nimenyamaza, sitafumbua kinywa changu,Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.
10 Uniondolee pigo lako;Kwa uadui wa mkono wako nimeangamia.