1 Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;Umenifanyizia nafasi wakati wa shida;Unifadhili na kuisikia sala yangu.
2 Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka?Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo?
3 Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa;BWANA atasikia nimwitapo.
4 Mwe na hofu wala msitende dhambi,Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
5 Toeni dhabihu za haki,Na kumtumaini BWANA.
6 Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema?BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.