1 Heri amkumbukaye mnyonge;BWANA atamwokoa siku ya taabu.
2 BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,Naye atafanikiwa katika nchi;Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.
3 BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.Katika ugonjwa wake umemtandikia.
4 Nami nalisema, BWANA, unifadhili,Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.
5 Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,Atakufa lini, jina lake likapotea?
6 Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,Moyo wake hujikusanyia maovu,Naye atokapo nje huyanena.