1 Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji.Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
2 Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai,Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku,Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.
4 Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu,Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano,Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu,Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.