7 Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maboromoko ya maji yako,Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.
8 Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami,Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.
9 Nitamwambia Mungu, mwamba wangu, Kwa nini umenisahau?Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
10 Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu,Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?