17 Haya yote yametupata, bali hatukukusahau,Wala hatukulihalifu agano lako.
18 Hatukuiacha mioyo yetu irudi nyuma,Wala hatua zetu hazikuiacha njia yako.
19 Hata utuponde katika kao la mbwa-mwitu,Na kutufunika kwa uvuli wa mauti.
20 Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu,Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu;
21 Je! Mungu hatalichunguza neno hilo?Maana ndiye azijuaye siri za moyo.
22 Hasha! Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;Tunafanywa kondoo waendao kuchinjwa.
23 Amka, Bwana, mbona umelala?Ondoka, usitutupe kabisa.