20 Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu,Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu;
21 Je! Mungu hatalichunguza neno hilo?Maana ndiye azijuaye siri za moyo.
22 Hasha! Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;Tunafanywa kondoo waendao kuchinjwa.
23 Amka, Bwana, mbona umelala?Ondoka, usitutupe kabisa.
24 Mbona unatuficha uso wako,Na kusahau kuonewa na kudhulumiwa kwetu?
25 Maana nafsi yetu imeinama mavumbini,Tumbo letu limegandamana na nchi.