6 Maana sitautumainia upinde wangu,Wala upanga wangu hautaniokoa.
7 Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu;Na watuchukiao umewaaibisha.
8 Tumejisifia Mungu mchana kutwa,Na jina lako tutalishukuru milele.
9 Lakini umetutupa, umetufedhehesha,Wala hutoki na majeshi yetu.
10 Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,Na watuchukiao wanajipatia mateka.
11 Umetutoa kama kondoo tuwe chakula,Na kututawanya kati ya mataifa.
12 Wawauza watu wako bila kupata mali,Wala hukupata faida kwa thamani yao.