8 Tumejisifia Mungu mchana kutwa,Na jina lako tutalishukuru milele.
9 Lakini umetutupa, umetufedhehesha,Wala hutoki na majeshi yetu.
10 Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,Na watuchukiao wanajipatia mateka.
11 Umetutoa kama kondoo tuwe chakula,Na kututawanya kati ya mataifa.
12 Wawauza watu wako bila kupata mali,Wala hukupata faida kwa thamani yao.
13 Umetufanya kuwa lawama kwa jirani zetu,Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.
14 Umetufanya kuwa mithali kwa mataifa,Sababu ya kutikisa kichwa kwa watu wa nchi.