2 Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu;Neema imemiminiwa midomoni mwako,Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.
3 Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari,Utukufu ni wako na fahari ni yako.
4 Katika fahari yako usitawi uendeleeKwa ajili ya kweli na upole na hakiNa mkono wako wa kuumeUtakufundisha mambo ya kutisha.
5 Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako;Imo mioyoni mwa adui za mfalme.
6 Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
7 Umeipenda haki;Umeichukia dhuluma.Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta,Mafuta ya furaha kuliko wenzako.
8 Mavazi yako yote hunukia manemaneNa udi na mdalasini.Katika majumba ya pembeVinubi vimekufurahisha.