9 Binti za wafalme wamoMiongoni mwa akina bibi wako wastahiki.Mkono wako wa kuume amesimama malkiaAmevaa dhahabu ya Ofiri.
10 Sikia, binti, utazame, utege sikio lako,Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.
11 Naye mfalme atautamani uzuri wako,Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.
12 Na binti Tiro analeta kipawa chake,Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako.
13 Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu,Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.
14 Atapelekwa kwa mfalmeNa mavazi yaliyofumwa kwa uzuri.Wanawali wenzake wanaomfuata,Watapelekwa kwako.
15 Watapelekwa kwa furaha na shangwe,Na kuingia katika nyumba ya mfalme.