1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3 Maji yake yajapovuma na kuumuka,Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
4 Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.