5 Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa;Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
6 Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki;Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka.
7 BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8 Njoni myatazame matendo ya BWANA,Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia;Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu,Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.