1 Sikieni haya, enyi mataifa yote;Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani.
2 Watu wakuu na watu wadogo wote pia,Tajiri na maskini wote pamoja.
3 Kinywa changu kitanena hekima,Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.
4 Nitatega sikio langu nisikie mithali,Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi
5 Kwa nini niogope siku za uovu,Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
6 Wa hao wanaozitumainia mali zao,Na kujisifia wingi wa utajiri wao;