2 Watu wakuu na watu wadogo wote pia,Tajiri na maskini wote pamoja.
3 Kinywa changu kitanena hekima,Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.
4 Nitatega sikio langu nisikie mithali,Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi
5 Kwa nini niogope siku za uovu,Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
6 Wa hao wanaozitumainia mali zao,Na kujisifia wingi wa utajiri wao;
7 Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake,Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,
8 (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama,Wala hana budi kuiacha hata milele;)