4 Nitatega sikio langu nisikie mithali,Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi
5 Kwa nini niogope siku za uovu,Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
6 Wa hao wanaozitumainia mali zao,Na kujisifia wingi wa utajiri wao;
7 Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake,Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,
8 (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama,Wala hana budi kuiacha hata milele;)
9 ili aishi sikuzote asilione kaburi.
10 Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa;Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja,Na kuwaachia wengine mali zao.