6 Wa hao wanaozitumainia mali zao,Na kujisifia wingi wa utajiri wao;
7 Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake,Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,
8 (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama,Wala hana budi kuiacha hata milele;)
9 ili aishi sikuzote asilione kaburi.
10 Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa;Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja,Na kuwaachia wengine mali zao.
11 Makaburi ni nyumba zao hata milele,Maskani zao vizazi hata vizazi.Hao waliotaja mashamba yaoKwa majina yao wenyewe.
12 Lakini mwanadamu hadumu katika heshima,Bali amefanana na wanyama wapoteao.