1 Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu,Ukuangalie kutafakari kwangu.
2 Uisikie sauti ya kilio changu,Ee Mfalme wangu na Mungu wangu,Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.
3 BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu,Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
4 Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya;Mtu mwovu hatakaa kwako;
5 Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako;Unawachukia wote watendao ubatili.
6 Utawaharibu wasemao uongo;BWANA humzira mwuaji na mwenye hila
7 Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako,Nitaingia nyumbani mwako;Na kusujudu kwa kicho,Nikilielekea hekalu lako takatifu.