3 BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu,Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
4 Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya;Mtu mwovu hatakaa kwako;
5 Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako;Unawachukia wote watendao ubatili.
6 Utawaharibu wasemao uongo;BWANA humzira mwuaji na mwenye hila
7 Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako,Nitaingia nyumbani mwako;Na kusujudu kwa kicho,Nikilielekea hekalu lako takatifu.
8 BWANA, uniongoze kwa haki yako,Kwa sababu yao wanaoniotea.Uisawazishe njia yako mbele ya uso wangu,
9 Maana vinywani mwao hamna uaminifu;Mtima wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi,Ulimi wao hujipendekeza.