1 Mungu, Mungu BWANA, amenena, ameiita nchi,Toka maawio ya jua hata machweo yake.
2 Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri,Mungu amemulika.
3 Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza,Moto utakula mbele zake,na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.
4 Ataziita mbingu zilizo juu,Na nchi pia awahukumu watu wake.
5 Nikusanyieni wacha Mungu wanguWaliofanya agano nami kwa dhabihu.
6 Na mbingu zitatangaza haki yake,Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.