13 Je! Nile nyama ya mafahali!Au ninywe damu ya mbuzi!
14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru;Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
15 Ukaniite siku ya mateso;Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
16 Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia,Una nini wewe kuitangaza sheria yangu,Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
17 Maana wewe umechukia maonyo,Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye,Ukashirikiana na wazinzi.
19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya,Na ulimi wako watunga hila.