15 Ukaniite siku ya mateso;Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
16 Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia,Una nini wewe kuitangaza sheria yangu,Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
17 Maana wewe umechukia maonyo,Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye,Ukashirikiana na wazinzi.
19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya,Na ulimi wako watunga hila.
20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako,Na mwana wa mama yako umemsingizia.
21 Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza;Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.Walakini nitakukemea;Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.