18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye,Ukashirikiana na wazinzi.
19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya,Na ulimi wako watunga hila.
20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako,Na mwana wa mama yako umemsingizia.
21 Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza;Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.Walakini nitakukemea;Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
22 Yafahamuni hayo,Ninyi mnaomsahau Mungu,Nisije nikawararueni,Asipatikane mwenye kuwaponya.