2 Ee Mungu, uyasikie maombi yangu,Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
3 Kwa maana wageni wamenishambulia;Watu watishao wananitafuta nafsi yangu;Hawakumweka Mungu mbele yao.
4 Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia;Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
5 Atawarudishia adui zangu ubaya wao;Uwaangamize kwa uaminifu wako.
6 Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu;Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.