1 Ee Mungu, uisikilize sala yangu,Wala usijifiche nikuombapo rehema.
2 Unisikilize na kunijibu,Nimetanga-tanga nikilalama na kuugua.
3 Kwa sababu ya sauti ya adui,Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu.Kwa maana wananitupia uovu,Na kwa ghadhabu wananiudhi.
4 Moyo wangu unaumia ndani yangu,Na hofu za mauti zimeniangukia.