12 Kwa maana aliyetukana si adui;Kama ndivyo, ningevumilia.Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye;Kama ndivyo, ningejificha asinione.
13 Bali ni wewe, mtu mwenzangu,Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.
14 Tulipeana shauri tamu; na kutembeaNyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.
15 Mauti na iwapate kwa ghafula,Na washuke kuzimu wangali hai,Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.
16 Nami nitamwita Mungu,Na BWANA ataniokoa;
17 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua,Naye ataisikia sauti yangu.
18 Ameiokoa nafsi yangu iwe salama, asinikaribie mtu,Maana walioshindana nami walikuwa wengi.