15 Mauti na iwapate kwa ghafula,Na washuke kuzimu wangali hai,Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.
16 Nami nitamwita Mungu,Na BWANA ataniokoa;
17 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua,Naye ataisikia sauti yangu.
18 Ameiokoa nafsi yangu iwe salama, asinikaribie mtu,Maana walioshindana nami walikuwa wengi.
19 Mungu atasikia na kuwajibu;Ndiye Yeye akaaye tangu milele.Mageuzi ya mambo hayawapati hao,Kwa hiyo hawamchi Mungu.
20 Amenyosha mkono awadhuru waliopatana naye,Amelihalifu agano lake.
21 Kinywa chake ni laini kuliko siagi,Bali moyo wake ni vita.Maneno yake ni mororo kuliko mafuta,Bali hayo ni panga wazi.