4 Moyo wangu unaumia ndani yangu,Na hofu za mauti zimeniangukia.
5 Hofu na tetemeko limenijia,Na hofu kubwa imenifunikiza.
6 Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa,Ningerukia mbali na kustarehe.
7 Ningekwenda zangu mbali,Ningetua jangwani.
8 Ningefanya haraka kuzikimbiaDhoruba na tufani.
9 Ee Bwana, uwaangamize, uzichafue ndimi zao,Maana nimeona dhuluma na fitina katika mji.
10 Mchana na usiku huzunguka kutani mwake;Uovu na taabu zimo ndani yake;