8 Ningefanya haraka kuzikimbiaDhoruba na tufani.
9 Ee Bwana, uwaangamize, uzichafue ndimi zao,Maana nimeona dhuluma na fitina katika mji.
10 Mchana na usiku huzunguka kutani mwake;Uovu na taabu zimo ndani yake;
11 Tamaa mbaya zimo ndani yake;Dhuluma na hila haziondoki mitaani mwake.
12 Kwa maana aliyetukana si adui;Kama ndivyo, ningevumilia.Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye;Kama ndivyo, ningejificha asinione.
13 Bali ni wewe, mtu mwenzangu,Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.
14 Tulipeana shauri tamu; na kutembeaNyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.