1 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,Mchana kutwa ananionea akileta vita.
2 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi.
3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;
4 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;Mwenye mwili atanitenda nini?
5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu,Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.