6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu,Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.
7 Je! Wataokoka kwa uovu wao?Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.
8 Umehesabu kutanga-tanga kwangu;Uyatie machozi yangu katika chupa yako;(Je! Hayamo katika kitabu chako?)
9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo.Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;
10 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.
11 Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini?
12 Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu;Nitakutolea dhabihu za kushukuru.