1 Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?
2 Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;Katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.
3 Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao;Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
4 Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka;Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.