5 Asiyeisikiliza sauti ya waganga,Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.
6 Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao;Ee BWANA, uyavunje magego ya wana-simba.
7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi;Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.
8 Kama konokono ayeyukaye na kutoweka,Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,
9 Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba,Ataipeperusha kama chamchela,Iliyo mibichi na iliyo moto.
10 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi;Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.