6 Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa,Na kuzunguka-zunguka mjini.
7 Tazama, kwa vinywa vyao huteuka,Midomoni mwao mna panga,Kwa maana ni nani asikiaye?
8 Na Wewe, BWANA, utawacheka,Utawadhihaki mataifa yote.
9 Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe,Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu
10 Mungu wa fadhili zangu atanitangulia,Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu.
11 Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau;Uwatawanye kwa uweza wako,Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu.
12 Kwa dhambi ya kinywa chao,Na kwa neno la midomo yao,Wanaswe kwa kiburi chao,Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao.