4 BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu,Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5 Maana mautini hapana kumbukumbu lako;Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
6 Nimechoka kwa kuugua kwangu;Kila usiku nakieleza kitanda changu;Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu.
7 Jicho langu limeharibika kwa masumbufu,Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.
8 Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu;Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
9 BWANA ameisikia dua yangu;BWANA atayatakabali maombi yangu.