8 Moabu ni bakuli langu la kunawia.Nitamtupia Edomu kiatu changu,Na kumpigia Filisti kelele za vita.
9 Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma?Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?
10 Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?
11 Utuletee msaada juu ya mtesi,Maana wokovu wa binadamu haufai.