4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
5 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
6 Ninapokukumbuka kitandani mwangu,Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku.
7 Maana Wewe umekuwa msaada wangu,Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
8 Nafsi yangu inakuandama sana;Mkono wako wa kuume unanitegemeza.
9 Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu,Wataingia pande za nchi zilizo chini.
10 Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga,Watakuwa riziki za mbwa-mwitu.