3 Ingawa maovu mengi yanamshinda,Wewe utayafunika maasi yetu.
4 Heri mtu yule umchaguaye,Na kumkaribisha akae nyuani mwako.Na tushibe wema wa nyumba yako,Patakatifu pa hekalu lako.
5 Kwa mambo ya kutisha utatujibu,Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu.Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia,Na la bahari iliyo mbali sana,
6 Milima waiweka imara kwa nguvu zako,Huku ukijifunga uweza kama mshipi.
7 Wautuliza uvumi wa bahari,Uvumi wa mawimbi yake,Na ghasia ya mataifa;
8 Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako;Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
9 Umeijilia nchi na kuisitawisha,Umeitajirisha sana;Mto wa Mungu umejaa maji;Wawaruzuku watu nafakaMaana ndiwe uitengenezaye ardhi.