8 Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako;Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
9 Umeijilia nchi na kuisitawisha,Umeitajirisha sana;Mto wa Mungu umejaa maji;Wawaruzuku watu nafakaMaana ndiwe uitengenezaye ardhi.
10 Matuta yake wayajaza maji;Wapasawazisha palipoinuka,Wailainisha nchi kwa manyunyu;Waibariki mimea yake.
11 Umeuvika mwaka taji ya wema wako;Mapito yako yadondoza unono.
12 Huyadondokea malisho ya nyikani,Na vilima vyajifunga furaha.