1 Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
2 Imbeni utukufu wa jina lake,Tukuzeni sifa zake.
3 Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini!Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako,Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
4 Nchi yote itakusujudia na kukuimbia,Naam, italiimbia jina lako.
5 Njoni yatazameni matendo ya Mungu;Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu;
6 Aligeuza bahari ikawa nchi kavu;Katika mto walivuka kwa miguu;Huko ndiko mlikomfurahia.
7 Atawala kwa uweza wake milele;Macho yake yanaangalia mataifa;Waasio wasijitukuze nafsi zao.