12 Uliwapandisha watuJuu ya vichwa vyetu.Tulipita motoni na majini;Ukatutoa na kutuleta kunako wingi.
13 Nitaingia nyumbani mwako na kafara;Nitaondoa kwako nadhiri zangu;
14 Ambazo midomo yangu ilizinena;Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni.
15 Kafara za vinono nitakutolea,Pamoja na fukizo la kondoo waume,Nitatoa ng’ombe pamoja na mbuzi.
16 Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu,Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
17 Nalimwita kwa kinywa changu,Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.
18 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu,Bwana asingesikia.