8 Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu,Itangazeni sauti ya sifa zake;
9 Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai,Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe.
10 Kwa maana umetupima, Ee Mungu,Umetujaribu inavyojaribiwa fedha.
11 Ulituingiza ndani ya wavu,Na kuweka viunoni mwetu mzigo uliotulemea.
12 Uliwapandisha watuJuu ya vichwa vyetu.Tulipita motoni na majini;Ukatutoa na kutuleta kunako wingi.
13 Nitaingia nyumbani mwako na kafara;Nitaondoa kwako nadhiri zangu;
14 Ambazo midomo yangu ilizinena;Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni.