30 Mkemee mnyama wa manyasini;Kundi la mafahali, na ndama za watu;Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha,Uwatawanye watu wapendao vita.
31 Masheki watakuja kutoka Misri,Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara.
32 Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu,Msifuni Bwana kwa nyimbo.
33 Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele;Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu.
34 Mhesabieni Mungu nguvu;Enzi yake i juu ya Israeli;Na nguvu zake zi mawinguni.