31 Masheki watakuja kutoka Misri,Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara.
32 Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu,Msifuni Bwana kwa nyimbo.
33 Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele;Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu.
34 Mhesabieni Mungu nguvu;Enzi yake i juu ya Israeli;Na nguvu zake zi mawinguni.