23 Macho yao yatiwe giza wasione,Na viuno vyao uvitetemeshe daima.
24 Uimwage ghadhabu yako juu yao,Na ukali wa hasira yako uwapate.
25 Matuo yao na yawe ukiwa,Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao.
26 Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe,Wanasimulia maumivu ya hao uliowatia jeraha.
27 Uwaongezee uovu juu ya uovu,Wala wasiingie katika haki yako.
28 Na wafutwe katika chuo cha uhai,Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe.
29 Nami niliye maskini na mtu wa huzuni,Mungu, wokovu wako utaniinua.