26 Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe,Wanasimulia maumivu ya hao uliowatia jeraha.
27 Uwaongezee uovu juu ya uovu,Wala wasiingie katika haki yako.
28 Na wafutwe katika chuo cha uhai,Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe.
29 Nami niliye maskini na mtu wa huzuni,Mungu, wokovu wako utaniinua.
30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,Nami nitamtukuza kwa shukrani.
31 Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng’ombe,Au ndama mwenye pembe na kwato.
32 Walioonewa watakapoona watafurahi;Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.